Sunday, May 3, 2020

#NINOGESHE_MPENZI! SIRI YA RAHA KITANDANI


WANAWAKE na WANAUME wametofautiana vikali kuhusu muda ambao MUME anapaswa kuchukua kutekeleza tendo la ndoa.
Huku WANAWAKE wakisema kwamba MUME anapaswa kuchukua dakika zaidi ya kumi na mbili, WANAUME hushikilia shughuli hii hutegemea mambo tofauti ikiwa ni pamoja na mazingira ambayo tendo linafanyiwa na makeke ya MWANAMKE.
Hata hivyo, muda ambao MWANAMUME anafaa kuchukua kukamilisha shughuli hutegemea hali ya yake ya kisaikolojia, anavyojiamini, hali yake ya afya na maandalizi kabla ya kipindi cha ngoma chumbani.
Ni kweli kumekuwa na mdahalo kuhusu muda ambao MWANAMUME anafaa kuchukua kabla ya kushusha mzigo wakati wa tendo la ndoa. Ni kweli WANAWAKE huwa wanatarajia mengi kutoka kwa WANAUME wakati wa shughuli na ni kweli ni WANAUME wachache wanaochukua muda wa zaidi ya dakika kumi kwenye burudani chumbani .
MUDA wa kawaida ambao MWANAMUME anapaswa kuchukua katika tendo la ndoa ni dakika sita.
Kumekuwa na hekaya nyingi kuhusu muda ambao Wanaume wanafaa kuchukua kutekeleza tendo la ndoa. Hekaya hizi zimepotosha watu na kuwafanya watarajie mengi kutoka kwa Waume wao. Kwa sababu ya habari hizi na matarajio yasiyoweza kuafikiwa, ndoa nyingi zimevunjika Wanawake wakilalama kwamba Wanaume wao hawawaridhishi chumbani.
Anasema tendo la ndoa ni sanaa ambayo utamu wake unatokana na maandalizi na utekelezaji wake na sio muda ambao mhusika mmoja anapaswa kuchukua. Hata hivyo tukiri kwamba Wanaume wengi wamepungukiwa na nguvu za kula uroda na kushindwa kabisa kudumu hata kwa dakika moja kwenye shughuli.
Tafiti zimeonyesha kuwa Wanaume wengi wamepungukiwa na nguvu za kiume na kuwafanya wasidumu hata sekunde kumi kwenye ngoma chumbani. Hali hii husababishwa na mambo tofauti kama vile mitindo ya maisha, mfadhaiko, maradhi kama vile msukumo wa damu, kisukari na msongo wa mawazo.
WANAUME hawana muda wa kufanya mazoezi na hata kujiandaa kwa tendo la ndoa wakiwa na wake zao.
Ukosefu wa maandalizi, mazoezi na mawasiliano kati ya Wanandoa kumechangia Wanaume kushindwa kujimudu wakati wa burudani chumbani na kushusha hata kabla ya wake wao kuridhika. Hii imekuwa ikiwaacha Wanawake wengi wakitamani ngoma zaidi. Ajabu ni kwamba ni tatizo ambalo linaonekana kuwa na Wanaume wa rika zote,
Ukosefu wa ubunifu na makeke kutoka kwa Wake wao pia kunachangia hali hii.
Mchango wa Mwanamke kwenye shughuli unamchamgamsha Mwanamume na kumtia ari na hamasa ya kushiriki ngoma. Makeke ya mwanamke huwa yanatia nakshi tendo la ndoa na Mwanaume anaweza kuchukua muda mrefu na pia kurudia raundi kadhaa , siri ya raha ni uhusiano wake na mtu wake.
Wanandoa wakiwa na uhusiano na mawasiliano bora, wanaelewana vyema bila ugomvi na Mume akipata lishe bora na kufanya mazoezi, basi wanaweza kuridhishana bila kujali muda ambao MUME anachukua kusoma katiba😁😁😁😁😁😁😁😁😁🙏
Nguvu zapungua
Kote ulimwenguni, watu wamepungukiwa na nguvu za kula uroda na wanahusisha hali hii na mitindo ya maisha na mabadiliko ya teknolojia yanayonyima Wanandoa muda wa kufanya mazoezi na kuwa pamoja.
Japo awali Wanaume walikuwa wakipungukiwa na nguvu za kula uroda umri unaposonga, hali imebadilika huku WANAUME wa kizazi cha sasa wakijikwaa kitandani na kufanya WANAWAKE kuwapachika jina la WANAUME wa kizazi cha sekunde tatu.
HAKUNA muda rasmi ambao MWANAMUME anafaa kuchukua kuridhisha Mwanamke chumbani bali inategemea ujuzi wa mtu wa kupandisha mzuka.
COPY& PASTE
NAOMI ANDREW


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/ninogeshempenzi-siri-ya-raha-kitandani.html

No comments:

Post a Comment