kijana kutoka Sumbawanga aliyekuja Dar es Salaam kumtafuta baba yake mzazi baada ya mama yake kushindwa kumsaidia ampate, Katika mihangaiko mingi kufanikisha azma yake jijini Dar, alikuja kukutana katika mazingira ya bahati tu na msichana anayetoka kwenye familia ya kitajiri inayoishi Masaki ambapo alisahau vitu vyake vya thamani lakini akavitunza na kuja kumkakadhi.
Wawili hao walijikuta wakipendana na msichana huyo kupata ujauzito ndani ya kipindi kifupi tu cha uhusiano wao. Hatua hiyo iliwafanya wafikirie kuurasimisha uhusiano wao kuwa ndoa.
Baada ya mazungumzo mengi katika familia ya msichana, kijana huyo naye alimuita mama yake kutoka Sumbawanga aliyefikia kwenye familia hiyo kwaajili ya kikao cha wazazi kupanga taratibu za ndoa. Kutano la mama yake na baba mkwe wake lilibadilisha hali ya hewa katika nyumba hiyo kwa kilichotokea.
Baada ya mazungumzo mengi katika familia ya msichana, kijana huyo naye alimuita mama yake kutoka Sumbawanga aliyefikia kwenye familia hiyo kwaajili ya kikao cha wazazi kupanga taratibu za ndoa. Kutano la mama yake na baba mkwe wake lilibadilisha hali ya hewa katika nyumba hiyo kwa kilichotokea.
Kijana huyo anasimulia kuwa mama yake alimuita jina baba wa msichana huyo na kusababisha mshtuko mkubwa.
“Kumbe yule baba mkwe wangu ni mzazi ambaye nilikuwa nikimtafuta kwa muda mrefu, ndiye baba yangu mzazi na ndiye yule aliyekuwa akiishi kule Namanyele akaja huku mjini kutafuta maisha na akaja akapata mke mwingine, akapata maisha yake hayo mazuri akazaa watoto wengine ambao ndiye mwanamke niliyempa ujauzito na ndiye mtoto wake wa pili yule nilisaidiana naye kule polisi,” amesimulia.
Anasema baada ya kufahamika ukweli huo mchungu, nyumba iligeuka kuwa ya vilio na mshtuko wa aina yake.
“Baba yangu pia analia kwa huzuni, hali imekuwa tafrani pale nyumbani haiwelewi. Kiukweli ikawa ni vilio, mimi nalia, mchumba wangu analia, mama, mama mkwe naye analia kwasababu limekuwa jambo la aibu pia kwamba mimi na yule mchumba wangu ni mtu na dada yake kabisa,” ameongeza.
Anasema ilichukua muda hadi hali ikatulia na wazazi wakaomba wapewe muda wa kujadiliana. Baada ya mazungumzo, baba yake alimuomba radhi mwanae kwa kumtelekeza, aliiomba pia radhi familia yake kwa kuwaficha kuwa alikuwa na familia nyingine.
Baba aliwasihi wana familia waitunze siri hiyo isitoke nje na kumtaka msichana akautoe ujauzito ili waanze kuishi kama kaka na dada. Anasema haikuwa rahisi wote kuukubali uamuzi huo kwakuwa uhusiano wao ulikuwa umechukua muda mrefu na walikuwa wanapendana sana.
Hali hiyo iliendelea kuwasumbua na kuwapa huzuni kubwa wasijue la kufanya. Anasema siku moja walienda kanisani na aliamua kusimulia mbele ya kanisa kisa kizima na mchungaji kueleza kuwa hayo ni makosa ya wazazi wao na kwamba kiumbe kilichokuwa tumboni hakipaswi kukatishwa maishja. Mchungaji pia aliamua kuwafungisha ndoa hapo hapo mbele ya kanisa na hadi leo wanaishi kama mume na mke.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/kijana-aliyezaa-na-kufunga-ndoa-na.html
No comments:
Post a Comment