Sunday, May 17, 2020

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WATU WA MKOANI NI HUU

Mrembo Jokate Kutumia Nafasi Yake Kutetea Wanawake na Watoto ...
Umeenda semina Dodoma, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Chamwino shukia St.Gaspar. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".
Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.
Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.
Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".
Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.
Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!
Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"
Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake.!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Hw basin" maji yanatoka!
Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa, unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.
Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu anachat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba - mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.
____
Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea ktk mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine kama tunavyotaka kutendewa.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/tofauti-ya-watu-wa-dar-na-watu-wa.html

No comments:

Post a Comment