Sunday, May 17, 2020

SIMULIZI FUPI:CHOCALATE ILOYOUA MTOTO WANGU.

Udaku Specially - Google Groups

Yapata mida ya mchana jua likiwa limetoa ndimi zake kuiramba ramba dunia hapa jijini dar hali ya joto ilikua juu sana.
Nikiwa ni daktari katika hospitali ya Temeke wodi namba tatu ya wanaume, siku hiyo nilichelewa kufanya "AROUND" ya kupitia wagonjwa wa wodi ile mpaka mida ya mchana bado nilikua sijamaliza zoezil lile.
Nilikuja kukatishwa baada ya kufika kwa mgonjwa aliyelala kitanda moja wapo pale wodini nilipomkuta anabubujikwa na machozi yasiyokawaida shuka aliyolalia ilikua imeloa tepetepe.Niliwajua vema wagonjwa waliokua wodi ile lakini yule aliyekua analia alikua mgeni kulazwa huku katundikiwa dripu
Wajibu wangu ulikua ni kujua Analia nini huwenda anasikia maumivu au kuzidiwa, sikuwa na budi kumfata
"shikamoo baba" nilimsalia kwani alionesha kanizidi umri zaidi ya miaka kumi na tano. Hakujibu chochote zaidi ya kuendelea kulia, Ukiona mwanaumea analia jua kuna jambo.
"Vipi baba unaumwa sana?" nilimuuliza nikiwa naangalia hali ya joto na mapigo ya moyo.
"Daktari naombeni mniruhusu niondoke kwangu" Sauti ya nzito ya kwikwi ikichanganyika na mpandisho wa mafua iliniambia.
"Kwanini tukuruhusu uende nyumbani angali leo ndio umeletwa, Umeambiwa una tatizo gani mpaka Kulazwa" Nilizidi kumuhoji kwani sikuangali faili lake nijue linasemaje.
"Sijaanza kulazwa leo hii ni siku ya tatu Niko hosptali"
"Mbona sijawahi kukuona?"
"Siku mbili zilizopita nilikua nimelazwa hosptali ya mwananyamala lakini wamenifanyia uhamisho leo asubuhi kwa matibabu zaidi katika hosptali yenu."
"nini zaidi?"
"Daktari Chocolate tu ndio imenifanya hivi" Aliposema hayo aliniangalia kidogo akaendele kabla sijamuhoji swali lingine.
" Unaweza kaaa nikakueleza kilichonitokea halafu nambie utanisaidiaje"
Niliangalia kwanza ile wodi kama kuna mgonjwa anayehitaji msaada ndipo nilipokubali kumsikiliza. Sheria ya pale hosptali sio sawa kwa daktari au ndugu wa mgonjwa
mgonjwa kukaa katika kitanda cha mgonjwa lakini nilikua radhi kuvunja sheria ile moyo ukinisikuma kumsikiliza na wala sikujua kwanini labda ni kwa ajili ya uzito wa ile story.
Hakuwa mgonjwa mahututi wa kutotoa sauti ya juu, nilipokaa pembeni yake alianza kunisimulia.
****
MIMI ni mfanyakazi wa TRA tena kitengo kizuri tu.Naishi kinondoni huko ndio nimebahatika kujenga nyumba baada ya kupambana siku nyingi.
Siku zote nimeishi na majirani zangu vizuri nikifurahi nao, nikicheka nao lakini sikujua kwamba maendeleo yangu yataniletea maadui wakubwa kiasi hiki.
Nyumba isiyokua na mwanamke itakua haijakamilika na ni pengo kubwa sana, nikaamua kuoa miaka kadhaa iliyopita.
Tumeishi na mke wangu kwa furaha.Lakini tatizo lilikua kwenye kupata mtoto kwani tulijaribu kipindi cha miaka miwili hatukubahatika kupata mtoto.
Jitihada za kuanza kutafuta suluhisho la tatizo letu likaanza. Na kwa kuwa nikijua napesa tulianza kuzunguka mahosptalini.
Mwishoni tulikuja kuambiwa tatizo liko kwa mke wangu na matibabu ya haraka yanahitajika, kwangu mbele ya pesa sio kitu cha umuhimu kuliko kupata mtoto. Nilikubali na pesa nikatoa matibabu ya yakaanza.
Ilipita miezi kadhaa baada ya matibabu tulipokuja kujaribu tena Kwa baraka za Mungu akashika mimba baada ya miezi tisa tukabahatika kupata mtoto wa kike tukamuita jina la Bahati kutokana na hali yenyewe.
Bahati alikua bahati kweli kwani hakuna alifikiri ipo siku tutakua na MTOTO lakini mungu pekee ndio anaejua.
Bahati akiwa ana miezi mitatu Mama yake akawa anasumbuliwa na tumbo kila mara ikafka sehemu hawezi kunyonyesha kisa kuumwa tumbo.
Nilimrejesha tena Hospatli ile ile tuliyotibiwa awali walipompima tena waligundua ana uvimbe wa kizazi.
Zilikua ni taarifa za kutisha kwetu hasa pale waliposema ili apone huo uvimbe unatakiwa utolewe kwa operesheni kubwa pia na kizazi chake kitatolewa kwani ndio kinachofanya awe na matatizo yote na kisipotelewa anaweza akaja akafa kwa kushikwa na magonjwa mengine ya kizazi.
Halikua wazo rahisi kulikubalia tukafikiri mchana usiku mke wangu akinigomea katu katu kutoa kizazi lakini hali ya tumbo ilipomzidi maumvu hakuwa na budi kufanyiwa operesheni hiyo akatolewa kizazi kuonesha hawezi zaa tena milele.
MTOTO tuliyekua nae ni mmoja WA kipekee malezi tuliyompa ni zaidi ya MTOTO kwani tulijua huyo ndio wa kwanza na wa mwisho.
Bahati alikua kama mmea baada ya kufikisha umri wa miezi nane alikua ashakua mkubwa mkubwa hata mimi baba yake nilikua nawezi kumtembeza.
Hela nilikua nazo lakini sikubahatika kununua gari wala ile nyumba sikuizungushia uzio. Nikawa na mazoea kila ninapotoka kazini jioni namkuta mke na mtoto wangu wako nje nami kwa furaha wote wawili na wabusu nakumchuku mtoto.
Kicheko kikubwa cha bahati kilikua pale ninaporudi kazini nakumchua alichokua anapenda na pia watoto wengi wanapenda ni kumurusha juu kama tulivyozoea wanaume wengi kuwarusha watoto wetu.
Yale mazoea ya kumrusha yalimea yakazidi mpaka akiwa na umri wa mwaka mmoja bado Tabia ya kutoka kazini nikiwakuta nje namrusha bahati sikuiacha.
Nakumbuka ilikua ndio juzi nikiwa njiani nimetoka kazini furha yangu kubwa ilikua ni kufika nyumbani kujumuika na familia yangu.
Nimezoea kusalimiana na kila mtu hakuna mtua ambaye hanijuj pale Kindondini japo nina uwezo wa kifedha sikutaka kuonesha dharau zangu sasa sjui kwanini. wamenifanyia hivi.
Nikiwa nishapita nyumba kadhaa karibu nifike kwangu Mbele yangu nilikutana NA MTOTO WA makamo kati ya miaka mitatu na nusu au minne wa kiume kashika Biskuiti mkononi.
Kalinisalinia tukaposhona lakini kabla sijapiga hatua kadhaa nilisikia kananiita
"Baba! Baba!" nilipogeuka alinioneshea ule mkono aliobeba biskuti
"Naomba nifungulie hii chokleti yangu" Nilitabasamu kidogo kuona mtoto mdogo kama yule anaomba msaada MTU asiyemjua lakini wanasema mtoto ni malaika.
Nilirudi nikamfungulia ile biskuti aina ya chocolate nikataka kumkbidhia lakini alikataa kwa kichwa
"Mama alinifundisha kama mtu akinisaidia kufungua bithikuti nimpe moja kama shukrani yangu, Kwa hiyo na wewe chukua moja" Kiukweli hakuna siku niliyocheka kwa kumuona mtoto mchangamfu na maneno ya kukonga nyoyo kama yule MTOTO.
Sikutaka kubishana nae nikachukua chocolate moja nikamrudishia pakti lake.
Nataka niondoke tena alinishika mkono
"Kula hapa hapa nkuone" hakika alifundishwa na mama yake tabia nzuri. Ujanja ulinishinda japo sikuzoea kula biskuti ya chokleti lakini siku hiyo ilibidi niile mbele yake ndipo akakubali niondokea bila kujua ile chokleti ndani yake ina nini.
Niliendelea NA safari ya kwenda kwangu dalili yoyote ya tukio baya haikuwepo.
Kama kawaida niliwakuta mke na mtoto wangu kibarazani nikafanya kama nilivyozoea kuwabusu wote wawili nikamchukua Bahati mtoto wangu nikana kumrusha juu juu.
Nilimrusha Mara ya kwanza,ya pili huku namchekesha mama yake akifurahia kitendo kile, mara ya tatu na ndio mara ya mwisho kumshika mwanangu, nilipomrusha Mara ya Nne juu Ghafla kwa juu nilpomrushia nikaona giza na kizunguzungu cha ghafla ata kabla mtoto sijamdaka nilijikuta naenda chini fahamu zikanipotea.
Leo hii nilipoletwa hapa Hosptali ndio nimepata nafuu ya kuamka, asubuhi ndugu walikuja kunitembelea wakaniambia habari ambazo zilinifanya niwe nalia toka mda ule mpaka sasa.
Kumbe siku ile wakati nilipoteza fahamu sikuwa ninemdaka mtoto, Kwa bahati mbaya Bahati MTOTO wangu wa kike wakipekee kwa kukosa mtu wakumdaka alidondoka kwa kichwa mpaka kwenye sakafu nakupasuka kichwa.
Hapa ninvyokwambia maneno haya wanafanya mpango wa mazishi ndio maana nimekuomba mniruhusu niondoke nyumbani hata nikaangalia mwili wa mtoto wangu kwa mara ya mwisho.
Inasemakana mwilini kwangu nikikula sumu sasa sumu gani ya aina ile nimekuja kukumbuka huwenda ni ile chocolate ya yule MTOTO katumwa kunifanyia vile bila yeye au mimi kujua na huyo mtu inaonesha anajua fika kuhusu ninavyorudigi na kumbeba
Tatizo ni kuwa nina kumbukumbu za tukio lile lakini sura ya yule mtoto siiumbuki kabisa mpaka sasa.
Kinachoniongezea Mimi machungu mke wangu atakua kwenye hali gani kwa sababu kizazi kashatolewa Tutapata wapi mtoto mwingine sisi.
*******
Alimaliza hiyo story akiwa anapiga kwikwi za kilio.Nilishangaa koti langu la udaktari linadondokewa na maji kuja kujishika usoni at a Mimi nilikua nalia.
Binadamu wa aina gani mwenye kumfanyia mwenzake ubaya kama huo tena kwa kumtuma MTOTO.?
***USIMUAMINI MWANADAMU YOYOTE*******MWISHO***
FUNZO: Mafanikio yako si kila mtu anayependa jaribu kufanya vitu kwa siri bila kuonekana na mwanadamu yeyote
Mwanadamu ni kama kinyonga nje ngozi ya kondooo ndani ana mwili wa MBWA MWITU....
Wengine wanakuchekea machoni lakini wana chuki moyoni. Usisahau kuweka namba nikuunge na group la Simuli za mazixha pia share na like kma zoote


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/simulizi-fupichocalate-iloyoua-mtoto.html

No comments:

Post a Comment