Friday, May 15, 2020

MLIOKO KWENYE MAHUSIANO/ NDOA TAFADHALINI NAOMBA MTAMBUE JAMBO HILI LA MSINGI.

Mwanaume lijali hawezi kuwa kwa mwanamke - Malaika | East Africa ...

Mahusiano yako ni tofauti na ya mtu mwingine, mtu wako ni tofauti na mtu mwingine. Kila mtu ana namna yake ya kupenda, si kila kitu kinachomtokea rafiki yako na wewe lazima kikutokee, si kila kitu ninachokiandika hapa kitakutokea na wewe. Najua kuna ambao mnasoma visa vyangu hapa na kupaniki, wengine kuogopa hata kuolewa, wengine hata kutaka kuachana na wapenzi wenu au kutoka katika ndoa zenu.
Hapana, si kwamba hakuna ndoa nzuri, si kwamba hakuna watu wenye furaha, wapo wengi tu lakini hatuwaandiki kwakua hawalalamiki? Naomba nifafanue, sidhani kama kuna mtu anaweza kununua vocha yake, akachukua muda wake na kunipigia simu kuanza kunielezea raha anazopata kwa mume au mke wake! Kwanza hatakua na muda huo kwa kua muda huo atakua anakla raha lakini hata mimi sitapata muda wa kumsikiliza.
Unaposoma kitu hapa, usikichukulie kama kilivyo, usipaniki, ukawehuka na kuona kama maisha yameshaisha. Hapana, kaa chuja, angalia kitu flani kimemtokea mwenzangu hembu na mimi nijifunze kwake! Nimeona dalili flani kwa mtu wangu hembu na mimi nijikinge yasijekunikuta, siandiki li uachane na mtu wako bali naandika ili ujifunze yasijekukukuta, kwamba yakianza kutokea uwe unajua nini chakufanya.
Acha kuishi kwa wasiwasi, maisha ni matamu, inawezekana hujafikia huyo utamu bado lakini nikuhakikishie upo!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/05/mlioko-kwenye-mahusiano-ndoa.html

No comments:

Post a Comment