Raia wa Nigeria walioshiriki “Kuchakachua” matokeo ya Uchaguzi wa Majimbo hawataruhusiwa kuingia nchini Marekani baada ya kuwekewa vikwazo
Imeelezwa kuwa Uchaguzi uliofanyika mwaka jana katika Majimbo ya Kogi na Bayelsa haukuwa wa Kidemokrasia hivyo matokeo yake yalivurugwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Michael Pompeo aliyetangaza marufuku hiyo hajaweka wazi majina ya waliowekewa vikwazo hivyo
Marekani imetumia nafasi hiyo kutangaza kuendelea kuunga mkono michakato ya Kidemokrasia katika chaguzi na kukemea vurugu zozote zenye lengo la kuharibu Uchaguzi
source http://www.bongoleo.com/2020/09/15/marekani-yawawekea-vikwazo-walioshiriki-kuvuruga-uchaguzi-wa-majimbo-nchini-nigeria/
No comments:
Post a Comment