Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa Afya.
Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo;
Zinazobamba ni pamoja na Lissu kuonywa,n Heche asema atakubali matokeo na Gwajima adai hana njaa atoa ahadi kedekede Kawe. Karibu
LISSU AONYWA
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde amewaonya wagombea wa vyama vya upinzani waache kutumia muda mwingi kueneza uongo na kumshambulia mgombea wa CCM, John Magufuli.
Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dodoma, Lusinde alimnyoshea kidole mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu akimweleza kuwa anapaswa kuzungumzia sera na kuwaelezea atawafanyia nini wananchi badala ya kutumia kampeni kumshambulia Magufuli.
Soma zaidi>>>
HECHE ADAI ATAKUBALI MATOKEO
MGOMBEA ubunge Jimbo la Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) amesema yupo tayari kukubali matokeo ya kuzidiwa kura na mpinzani wake, Mwita Waitara (CCM) endapo haki na uwazi utatendeka.
Kauli hiyo aliitoa juzi kwenye mkutano wa uzinduzi kampeni kwenye Jimbo la Tarime Vijijini, uliofanyika Kata ya Sirari ambapo wagombea wengine, Julius Mwita (Musoma Mjini), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Ester Matiko (Tarime Mjini), Ezekiah Wenje (Rorya), Catherine Ruge (Serengeti) walihudhuria na kuwataka wananchi kutofanya kosa la kumchagua Waitara kwa kuwa ni msaliti na hana msimamo.
Soma zaidi>>>
ASEMA HANA NJAA
ASKOFU Josephat Gwajima, mgombea ubunge katika Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema alianza kuitumikia Kawe siku nyingi.
Amesema, kabla ya kuwa mbunge, tayari wakazi wa Salasala 250 na misikiti saba imeneemeka kwa kuunganishia maji kwa fedha zake mwenyewe.
Na kwamba, kazi ya ubunge anayoimba kutoka kwa wananchi, si ya kuganga njaa bali kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo tu.
Soma zaidi>>>
source http://www.bongoleo.com/2020/09/07/dondoo-za-leo-lissu-aonywa-asema-atakubali-matokeo/
No comments:
Post a Comment