Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u Bukheri wa Afya
Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.
Zinazobamba ni pamoja na Lissu ageukia vigogo, Mwakyembe asema yamekwisha na Majaliwa ataja sifa za kupigiwa kura. Endelea kubaki katika ukurasa huu uspate kujua undani wa habari hizi.
LISSU AGEUKIA VIGOGO
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameahidi kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa umiliki wa ardhi nchini, akidai kubaini vigogo wengi wamejimilikisha mashamba makubwa.
Lissu alitoa ahadi hiyo jana wakati akiendelea na kampeni zake za uchaguzi mkuu wilayani Ifakara mkoani Morogoro, akiwaambia wananchi kuwa kuna vigogo nchini wamejimilisha mashamba makubwa hususan mkoani huko.
“Wakubwa hawa wametumia madaraka yao vibaya kiufisadi, wameiba ardhi ya wananchi, wananchi wanahangaika, hawana ardhi kidogo ya kulima mazao wapate chakula, maelfu ya hekta yamekaa bure kwa sababu wakubwa wameyachukua,” alidai.
Soma zaidi>>>
MWAKYEMBE ASEMA YAMEKWISHA
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutambua kwamba kura za maoni zilishakwisha na kazi iliyobaki ni kusaka kura za kutosha kwa wagombea wateule wa chama kwa ngazi ya urais, ubunge na udiwani.
Juzi, katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Kyela alilokuwa mbunge wake, Dk. Mwakyembe alisema huu siyo muda wa malumbano, bali kusaka ushindi wa CCM kwa nafasi zote tatu kwa udi na uvumba.
“Ukishampigia kura Rais Magufuli, piga kura yako ya pili kwa Ally Mlaghila kwa nafasi ya ubunge na tatu kwa madiwani wa CCM kukamilisha mafiga matatu ya uongozi,” alisema.
Soma zaidi>>>
MJALIWA ATAJA SIFA ZA KUPIGIWA KURA
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa, amewataka wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba 28, mwaka huu kumchagua kiongozi mwenye uwezo wa kulinda tunu za taifa ikiwamo amani na muungano.
Alitoa rai hiyo jana alipomwombea kura mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli, mgombea ubunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu na wagombea udiwani kwa tiketi ya CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini.
Soma zaidi>>>
Kumalizia dondoo tuangazie suala hili la malezi
Baba unatakiwa utambue kwamba mtoto wako wa kike husikiliza kila neno na kuangalia mtazamo juu ya wanawake wengine.
Hivyo, kadri anvyokua hutumia maneno yako na mtazamo wako juu ya wanawake kujijengea thamani yake. #Dk.NormanJonastweet #Malezi #ElimikaWikiendi
source http://www.bongoleo.com/2020/09/13/dondoo-za-leo-lissu-ageukia-vigogo-mwakyembe-asema-yamekwisha-majaliwa-ataja-sifa/
No comments:
Post a Comment