Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.
Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.
Zinazobamba leo ni pamoja na Membe kutoa alivyofukuzwa CCM, na waziri alieyekua anaenda kunyoosha nguo huyu hapa ni nani? Na mwisho ni juu ya kodi na JPM , kulikoni? Karibu;
MEMBE ATAJA KILICHOMFUKUZISHA CCM
BERNARD Membe, mgombea urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, ameweka hadharani mambo manne yaliyosababisha kufukuzwa Chama Cha Mapindu (CCM).
Membe alifukuzwa CCM tarehe 28 Februari 2020 akituhumiwa kukiuka miongozo na taratibu ya chama hicho tangu mwaka 2014.
Jana Jumanne tarehe 1 Septemba 2020, akihutumia mamia ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni za urais uliofanyika uwanja wa Mpilipili Mjini Lindi, Membe amewaeleza wananchi hao wa kusini ikiwa ni mara ya kwanza kuzungumza mkasa huo kwenye mkutano.
Membe aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania tangu mwaka 2007 hadi 2015 enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete amesema, jambo la kwanza ni ubovu wa barabara za Kusini, “Tumechoka kutembea na mavumbi kana kwamba tunatoka mashambani kila siku.”
Pili, Membe ambaye ni Mshauri Mkuu wa ACT-Wazalendo amesema, ni dharau tunazofanyiwa watu wa Kusini, tunaonekana kama wajinga, watukanwe mashangazi zetu, hizo ni dharau ambazo hatupaswi kufanyiwi.
HUYU NDO WAZIRI ALIYEKUA ANAENDA KUNYOOSHA ULAYA NGUO
Waziri wa Katiba na Sheria, ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Dkt Mwigulu Nchemba, amesema kuwa miongoni mwa wagombea wanaojinadi kama ni watoto wa Singida siyo wazalendo kwa kuwa kuna mmoja alipokuwa Waziri alikuwa anaenda kunyosha Suti nje ya Nchi.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Mwigulu Nchemba.
Dkt Nchemba ametoa kauli hiyo jana Septemba 1, 2020, katika Uwanja wa Bombadier uliopo Mjini Singida, wakati mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiomba kura kwa wananchi wa Mkoa huo.
“Wengine wanakuja hapa wanajifanya eti ni watoto wa Singida hawana hata uzalendo, kuna mmoja Mh Rais tulikuwa Mawaziri wote hata Suti zake alikuwa anaenda kunyoosha Ulaya, anauchungu na Singida huyo!, wengine walikuwa wanasema Tanzania siyo salama sasa hivi wamekuja sababu advance wamechukua baada ya uchaguzi tu watasema siyo salama”, amesema Dkt Nchemba.
Aidha Dkt Nchemba ameongeza kuwa, “Ninyi Wana Singida niwaambieni Rais ni huyu Dkt Magufuli na kwa kuwa sisi ndiyo mtakuwa mnatutuma, niwaombe ihurumieni Tanzania wale wagombea wengine wote nawafahamu na nikiangalia janja janja yao hata advance walishachukua nchi yetu itauzwa”.
LAZIMA KODI ILIPWE
“Kuna Watu watasema tumenunua Ndege zinatusaidia nini!, hizi Ndege zinaleta Watalii ambao wanaleta fedha zinazosaidia kujenga Barabara nk, huwezi kutokea ukasema mkinichagua hamtolipa kodi hata enzi za mitume walilipa kodi, hata Ulaya wanalipa kodi na wana sheria ngumu kweli”-JPM
source http://www.bongoleo.com/2020/09/02/dondoo-za-leo-membe-ataja-kilichomfukuzisha-ccmalienda-ulaya-kunyoosha-nguo/
No comments:
Post a Comment