Monday, September 21, 2020

Dondoo za leo; ACT yamuunga mkono Lissu urais/Membe atokwa povu/ JPM asema sio lazima

Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u Bukheri wa Afya

Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na ACT kumuunga mkono Lissu, Membe akanusha na mwisho ni juu ya JPM kusema vitambulisho vya wajasiriamali sio lazima, kivipi? Karibu;

ACT WAZALENDO YAMUUNGA MKONO LISSU

Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad ametangaza chama chao kumuidhinisha Mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu kuwa mgombea wao wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Maalim Seif amesema hayo saa chache zilizopita akiwa kwenye Kampeni katika Jimbo la Donge

Msemaji wa ACT-Wazalendo ameithibitishia JamiiForums kuwa huu ndio msimamo wa chama

Mapema mwezi huu, Lissu alitangaza kumuunga mkono Maalim Seif akisema Chama cha ACT-Wazalendo kinaweza kuiondoa CCM madarakani visiwani Zanzibar

MEMBE AKANUSHA

Bernard Membe amekanusha taarifa za kuwa wamejiunga na CHADEMA katika ngazi ya Urais akiseme yeye ndio Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo

Membe amesema, “Mimi ndiyo Mgombea Urais wa JMT kupitia Chama cha ACT-Wazalendo. Mimi ndiye niliyekabidhiwa Ilani ya Chama hicho kuinadi kote nchini kwenye Uchaguzi huu”

Kauli yake inakuja baada ya Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad kumuidhinisha Tundu Lissu (CHADEMA) kuwa Mgombea wao wa Urais wa Tanzania

VITAMBULISHO VYA MACHINGA SIO LAZIMA


RAIS John Magufuli amewakemea baadhi ya wakuu wa wilaya wanaowalazimisha wafanyabiashara wadogo kununua vitambulisho, kwa kuwaeleza kuwa ni hiari kwa mfanyabiashara kuwa nacho au la.

Amesema serikali ilianzisha mchakato wa kuuza vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo kwa lengo la kuwasaidia kutosumbuliwa na askari mgambo wa jiji, pindi wanapouza bidhaa zao mitaani.

Alitoa kauli hiyo jana mkoani Tabora, wakati akizungumza na maelfu ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi waliojitokeza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, kumsikiliza akimwaga sera na kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kwa awamu ya pili kuwa rais.
]
“Vitambulisho havilazimishwi, elimu itolewe kwa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kuwa na vitambulisho hivyo. Tunatoa vitambulisho ili wafanyabiashara wasisumbuliwe, vitambulisho havitolewi kwa bunduki bali vinatolewa kwa Sh. 20,000,” alisema Rais Magufuli na kuongeza:

“DC (Mkuu wa Wilaya) wa hapa azingatie maelekezo haya. Kama kuna mfanyabiashara ambaye hataki kitambulisho aende kwa mgambo akamwagiwe chakula chake, anyang’anywe bidhaa zake. Ndiyo maana tukasema walipe kiasi hicho, ndiyo faida utafanya biashara popote, hayo ndiyo maagizo yangu.”



source http://www.bongoleo.com/2020/09/22/dondoo-za-leo-act-yamuunga-mkono-lissu-urais-membe-atokwa-povu-jpm-asema-sio-lazima/

No comments:

Post a Comment