Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u Bukheri wa Afya
Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.
Zinazobamba ni pamoja na Zitto kumsaliti Membe? Maalimu Seif amwita Lissu Zanzibar na CCM Lindi wamvaa Membe. Karibu;
ZITTO KUMSALITI MEMBE TAREHE 3?
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Vyama vya Upinzani nchini vimekubaliana kumuunga mkono Mgombea mmoja wa Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na pia, kwa upande wa Zanzibar
Zitto ameongeza kuwa, Oktoba 3, 2020 katika mkutano wa hadhara utakaohusisa CHADEMA, ACT-Wazalendo na Vyama vingine vya Upinzani watatangaza ni nani hasa atasimama kama Mgombea Urais
Amesema, ACT-Wazalendo wameshajadiliana na wameshawasilisha mapendekezo yao kwa CHADEMA na baada ya pande zote kukamilisha mazungumzo watatangaza makubaliano yatakayofikiwa
KUKUTANA NA LISSU
MAALIM Seif Sharif Hamad, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo anataka kukutana na Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema ili ampe mikakati ya ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.
Maalim Seif ambaye ni Mwenyekiti chama hicho ametoa kauli hiyo jana Jumanne tarehe 22 Septemba 2020 katika mkutano wake na timu za ushindi za mikoa na majimbo ACT-Wazaendo za Unguja.
Alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka mikakati yake ya kumtafutia ushindi Rais John Pombe Magufuli, Mgombea wake Urais wa Tanzania na kwamba Lissu anatakiwa awe na mbinu za kupangua mikakati hiyo.
“Kule bara kuna mikakati yao yote nimeshaambiwa na mimi nataka nikutane na Lissu nimpe mikakati hiyo na nimwambie akiweza kuzuia mikakati hiyo wamekwisha hawa,” alisema Maalim Seif.
WAMVAAA MEMBE
Kitendo cha mgombea wa urais anayepitia chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Bernard Membe kutoendelea kufanya mikutano ya kampeni kimetajwa kuwa ni dalili ya kushindwa kumudu gharama za uchaguzi.
Madebe ambaye alimsema mgombea huyo hafai kuchaguliwa kuwa Rais, alisema kitendo cha Membe kuzindua kampeni zake nakushindwa kuendelea ni dalili ya kushindwa kutokanana uwezo mdogo wa kumudu gharama za uchaguzi. Kwahiyo wanachama na wapenzi wa ACT- Wazalendo hawana budi kukubali kwamba mgombea wao amejitoa kimyakimya kwenye mbio za urais.
source http://www.bongoleo.com/2020/09/23/dondoo-za-leo-zitto-kumsaliti-membe-tarehe-3-maalim-seif-amwita-wazungumze-wamvaa/
No comments:
Post a Comment