Tuesday, September 15, 2020

Dondoo za leo; Membe: Tumepingwa nondo kuingiza pesa / Kenya yasalimu amri /Shana afariki dunia

Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u Bukheri wa Afya

Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba ni pamoja

WAMETUKIMBIA AISEEE!

BERNARD Membe, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesema, mazingira magumu ya siasa kwa sasa, yamesababisha marafiki na wafanyabiashara kushindwa kuwasaidia.

Na kwamba, kusuasua kwa kampeni hasa vyama vya upinzani nchini, kunatokana na ukweli kwamba, wagombea wengi wana ukata kwani hawana msaada tofauti na chaguzi zilizopita.

Membe amabye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Septemba 2020, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea Dubai.

“Mnapokuwa katika mbio za urais, unatakiwa ukae ujipange kifedha na uwe na timu za kampemi,  vyama vyote vyenye wagombea, wana ukata wa fedha sababu vyanzo vyetu vinavyokubalika kisheria, wafanyabiasha wanaotoa msaada wote wamekimbia, hatuna fedha,” amesema Membe.

Amesema, kikwazo kingine ni mazingira ya sasa ambayo hayaruhusu kutoa wala kuingiza fedha ndani ya nchi, jambo ambalo linasababisha ugumu wa kampeni.

KENYA YALAMBA NYAYO

Kenya siku ya jumanne imetoa orodha ya mataifa ambayo raia wake wanaruhiusiwa kuingiaa nchini bila kuhitajika kwenda karantini kwa siku 14 . Hatua ya hapo awali ya Kenya kuwahitaji watanzania kwenda karantini wanapowasili kenya iliifanya Tanzania kulipiga marufuku shirika la  safari za ndege nchini KQ dhidi ya kufanya safari zake hadi katika taifa hilo Jirani .

Kulegezwa kwa masharti hayo kuhusu karantini kunaashiria kwamba kenya ina matumaini kwamba visa vya ugonjwa wa corona katika nchi hizo vimethibitiwa . Tanzania haijakuwa ikitoa iaddi ya wagonjwa wa corona tangu mwezi Aprili na kuzua hofu miongoni mwa mataifa  mengine ya afrika mashariki kwamba utawala wa Rais Magufuli haujachukua hatua zifaazo kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo .

RPC SHANA AFARIKI

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Alifahamika zaidi katika kujihusisha na shughuli za Vyama akiwa na sare za kipolisi. Aidha, aliwahi kufananisha Chama Tawala, Serikali na Dola kwa Kanuni za Kihesabu.
Kamanda Shana aliwahi kuwa RCO Mikoa Mbalimbali Nchini ikiwemo Simiyu, RPC-Mikoa ya Pwani, Mwanza na Arusha.
ACP Jonathan Shana amefariki akiwa Afisa Mnadhimu Namba Moja katika Chuo cha Polisi (CCP) Moshi



source http://www.bongoleo.com/2020/09/16/dondoo-za-leo-membe-tumepingwa-nondo-kuingiza-pesa-kenya-yasalimu-amri-shana-afariki-dunia/

No comments:

Post a Comment