Wednesday, September 2, 2020

Dondoo za leo; Madhaifu 7 hoja za lissu, Ataka JPM aulizwe 4, Majaliwa amuombea kura

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo na ni madhaifu 7 hoja za Lissu, Membe ataka JPM aulizwe manne na mwisho ni juu ya Majaliwa kuomba kura kwa JPM

MADHAIFU 7 HOJA ZA LISSU

Kwanza nashukuru sasa kuona ndugu yangu Tundu Lissu ameanza kuleta hoja zinazoweza kuanza kujadilika kama mgombea, tofauti na mwanzo ambapo ilikuwa ni masimulizi ambayo hayakuwa na lolote kumsaidia uamuzi wa mpiga kura.

Agosti 30, mwaka huu, nilifuatilia hotuba yake iliyokosoa masuala kadhaa ambayo nimeona si busara ayatumie kupotosha Watanzania kufanya maamuzi katika misingi ya upotoshaji.

Ili kurahisisha, nimepanga mawazo yangu katika mafungu saba ninayoyaita matundu saba ya hoja za Lisu.

Mosi, Lissu anasema Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mwaka huu 2020 kuhusu urahisi wa kufanya Biashara (Easy of Doing Business Report 2020) imeishusha Tanzania kutokana na utawala wa Rais John Magufuli.

Asichokijua Lissu na wenzake wanaotumia hoja hiyo, ni kwamba tayari Benki ya Dunia (WB), katika taarifa yake ya Agosti 27, 2020, imeifuta tathmini hiyo ya mwaka 2020 na ile ya 2018.

Benki ya Dunia imeleza wazi kuwa tathimini hizo zilikuwa na kasoro nyingi za kiuweledi na hivyo kukosa uhalisia. Kwa maelezo zaidi soma https://www.worldbank.org/en/news/statement/2020/08/27/doing-business—data-irregularities-statement.

Pili, Lissu anashangaa inawezekanaje tuingie uchumi wa kati wakati tathimini ya taasisi ya Moodys imeonesha Tanzania imeshuka daraja kutoka B1 Mwaka 2017 kwenda B2 mwaka 2020 katika uwezo wa kukopa! (credit rating).

Soma zaidi>>>

MEMBE ATAKA JPM AULIZWE 4

BERNARD Membe, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, amewataka wananchi wa Kilwa Mkoa wa Lindi, kuumuuliza maswali manne, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais John Pombe Magufuli.

Mwanadiplomasia huyo, ameyatoa maswali hayo kwa wananchi wakati akihutubia mkutano wa kampeni za urais uliofanyika jana Jumatano tarehe 2 Septemba 2020 katika viwanja vya Bustani ya Mkapa, Kilwa Masoko.

Membe aliyepata kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania kati ya mwaka 2007 hadi 2015 enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema, Rais Magufuli atakapofika Kilwa aulizwe maswali hayo.

Soma zaidi>>>

MAJALIWA AMUOMBEA KURA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewaomba wananchi wa mkoa wa Arusha kumchagua Rais John Magufuli na wagombea wake wote wa ubunge na udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili waendelee kuleta maendeleo zaidi ya sasa waliyoyafanya ambayo dunia inashuhudia.

Akizungumza jana Mto wa Mbu wilayani Monduli, wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Frederick Lowassa, na Rais Magufuli, alisema ni vyema wapigakura wakachagua viongozi bora kupitia chama hicho na si vinginevyo.

“Sina mashaka (shaka) mtatupa kura zote kwa sababu serikali imefanya makubwa kama vile tumejenga vituo vya afya 498 nchini na vyote vina jengo la upasuaji na tumewapunguzia safari za kufuata huduma hizo mbali au wilayani,” alisema.

Majaliwa alisema kila wilaya vimejengwa vituo hivyo na bado wanahitaji kuongeza vituo hivyo, lakini wanahitaji kupata kura zote ili watekeleze hilo.

“Leo (jana) nitakabidhi Ilani ya CCM ili wananchi waone kazi tutakazozifanya, sasa naomba Fredrick beba kero zote za wananchi ili ukashughulike nazo,” alisema.

Mbali na ujenzi wa vituo vya afya, pia alisema wanajenga hospitali za wilaya na wanaendelea kujenga katika wilaya zote na kwamba serikali imeshatoa zaidi ya Sh. bilioni 2.5 za dawa kwenye hospitali na vituo vya afya, hivyo wanaomba kura ili waendelee kukamilisha waliyodhamiria.

“Muhimu zaidi mjue tumedhamiria kusomesha watoto wetu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Mnajua tumefuta michango ya ovyo ovyo shuleni leo mtoto anakwenda shuleni bila malipo ili zile fedha mlizokuwa mnatumia kwa michango, mtumie kwa mambo mengine,” alisema.

Katika kufanikisha hilo, alisema kila mwezi zaidi ya Sh. bilioni 24 zinatengwa kwa ajili ya shule za msingi na sekondari na pia wanapeleka fedha nyingi ili watoto wasome bila shida.



source http://www.bongoleo.com/2020/09/03/dondoo-za-leo-madhaifu-7-hoja-za-lissu-ataka-jpm-aulizwe-4-majaliwa-amuombea-kura/

No comments:

Post a Comment