Monday, September 14, 2020

Dondoo za leo; JPM ahairisha mkutano Kagera/ Walia kuchanwa mabango yao/ Akishinda kuondoa vitambulisho vya NIDA

Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u Bukheri wa Afya

Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba ni pamoja JPM kuhairisha mkutano, na walia mabango yao kuchanwa na mgombea urais

 

JPM AHAIRISHA MKUTANO KAGERA

Mkutano wa kampeni wa Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Magufuli ambao ilikuwa ufanyike mkoani Kagera kesho umeahirishwa hadi Jumatano Septemba 16, 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 14, 2020 Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa Hamimu Muhamud amesema mkutano huo umeahirishwa ili kuendelea kuboresha maandalizi ambayo hata hivyo amesema yamekamilika.

Amesema kuwa mgombea huyo ataingia mkoani Kagera kesho jioni ya Septemba 15,2020 akitokea wilayani Chato mkoani Geita.

Soma zaidi>>>

WALIA KUCHANWA MABANGO YAO

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga, kimelaani tabia ya baadhi ya vijana wanaodhaniwa kuwa ni wa upinzani kuchana mabango ya mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, alitoa malalamiko hayo jana wakati akizindua kampeni za CCM Jimbo la Shinyanga Mjini, zilizofanyika kwenye Kata ya Ngokolo, mjini humo.

Alisema tabia iliyoanza kufanywa na vijana wa upinzani kuchana mabango ya mgombea wao wa urais, Dk. John Magufuli, haitavumilika na atakayekamatwa atachukuliwa hatua kali.

“Naombeni vyama vya upinzani tufanyeni kampeni za kistaarabu ili uchaguzi uishe kwa amani sasa hivi kuna vijana wenu wameanza kuchana mabango ya mgombea wetu wa urais pamoja na kuyaandika maneno machafu hili siyo sawa,” alisema Mlolwa.

Soma zaidi>>>

AHAIDI KUFUTA VITAMBULISHO VYA TAIFA

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD), Mohamed Mazrui, amesema iwapo atapata ridhaa ya kuongoza Tanzania, serikali yake itafuta utaratibu wa wananchi kupewa Vitambulisho vya Taifa.

Alisema hayo juzi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam.
Mazrui alisema, baada ya kufuta utaratibu wa kutoa Vitambulisho vya Taifa, wananchi watapewa hati za kusafiria (passport) ambazo zitatolewa bure nchi nzima.

Alisema, hati hizo zitawawezesha wananchi hao kusafiri katika nchi yoyote kwa ajili ya kwenda kutafuta maisha, bila vikwazo vyovyote.

Soma zaidi>>>



source http://www.bongoleo.com/2020/09/15/dondoo-za-leo-jpm-ahairisha-mkutano-kagera-walia-kuchanwa-mabango-yao-akishinda-kuondoa-vitambulisho-vya-nida/

No comments:

Post a Comment