Habari yako mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa Afya.
Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo;
Zinazobamba ni pamoja na Lissu kufuta vitambulisho vya Machinga, JPM kupandisha Mishahara na Gwajima Aliamsha. Karibu usome upate kusoma habari hizi kwa kina.
LISSU KUFUTA VITAMBULISHO VYA MACHINGA
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameahidi kufuta utaratibu wa serikali kutoa vitambulisho maalum kwa wafanyabiashara ndogo, maarufu machinga, ikiwa atashinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Lissu alitoa ahadi hiyo jana kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe jijini Mbeya wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho Kanda ya Nyasa, akiahidi kujenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za kundi hilo ambayo yatakuwa wazi usiku na mchana.
“Tutafuta utaratibu wa kuwauzia wamachinga vitambulisho ambavyo vinatolewa sasa. Pamoja na kupewa vitambulisho hivyo, wanauza bidhaa zao kwenye mitaro na barabarani, jua linakuwa lao na mvua yao.
Soma zaidi>>>
MAGUFULI KUPANDISHA MISHAHARA
MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ameahidi kupandisha mishahara ya watumishi wa umma ndani ya miaka mitano ijayo ikiwa atashinda tena kuongoza nafasi hiyo.
Amesema hakutekeleza ahadi hiyo katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wake kwa kuwa alitaka kukamilisha kwanza baadhi ya mambo muhimu ya kitaifa ikiwamo ujenzi wa hospitali, zahanati, huduma ya elimu na miradi mingine ya maendeleo.
“Mtu anakuja anasema hatupandishi mishahara ya wafanyakazi, hivi ukimpandisha mtu daraja, mshahara wake unabaki palepale?
Soma zaidi>>>
GWAJIMA ALIAMSHA
WAKATI kampeni zikiendelea kupamba moto, mgombea ubunge wa Kawe (CCM), Askofu Josephat Gwajima, ameahidi kununua greda na maroli kwa fedha zake ili kutengeneza barabara za mitaa yote ya jimbo hilo ikiwa atashinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Pia, amesema atanunua magari ya wagonjwa na kuyasambaza jimboni ndani ya siku 90 baada ya kuchaguliwa, akitamba kuwa hahitaji kusubiri bajeti ya serikali.
“Mimi sijaja kufanya kazi hii kuganga njaa, acha hao wa upande ule ambao wanaomba ubunge kutumia fedha waliyokopa benki halafu baada ya miaka mitano wanaanza kurejesha marejesho na mpaka amalize marejesho atakuwa hana muda wa kukuletea maendeleo. Mimi sina marejesho ya kurejesha,” alitamba.
Soma zaidi>>>
Kumalizia dondoo, tuangazie suala la kuwaachia watoto wadogo vifaa vya kielektroniki
Kumekuwa na wimbi kuwa la watu kuwaachia watoto simu wachezee ama kwa kuwawekea video watazame huku wakiwa wamezishikilia au vyovyote vile. Je umshawahi kujiuliza kwamba yaweza kuwa na madhara kiafya?
Norman Jonas, Daktari na mtaalamu wa masuala ya afya ya Jamii anaesema sio vyema kwa Watoto chini ya miaka 3 kupewa vifaa vya kieletroniki km simu au tablet wachezee kwa zaidi ya saa 1 Kwa siku.
Anafafanua kuwa Tafiti zinaonyesha kuwa matumizi ya kupitiliza ya simu kwa watoto huathiri ukuaji wao wa akili hasa eneo la lugha, ufahamu na uelewa wa kijamii.
Ni hayo tu kwa leo mdau wetu, asante kwa kuendelea kuhabarika na Opera News na siku njema.
source http://www.bongoleo.com/2020/09/06/dondoo-za-leo-lissu-kufuta-vitambulisho-vya-machinga-jpm-kupandisha-mishahara-na-gwajima-aliamsha/
No comments:
Post a Comment