Saturday, April 4, 2020

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

HABARI NA MATUKIO: MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU ...


✍๐ŸฝUkichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. ๐Ÿ‘‰๐ŸพKatika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa ๐Ÿ™‡๐Ÿฝ๐Ÿ“š Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi ๐Ÿก na ๐Ÿš— ๐Ÿš™magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!) ๐Ÿ‘‰๐ŸพWapo ๐Ÿ™‡๐Ÿฝ๐Ÿ“šwasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana ๐Ÿ‘‰๐ŸพLakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga Hii inachangiwa na mambo mawili:- ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli ๐Ÿ‘‰๐ŸพHata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio ๐Ÿ‘‰๐ŸพKadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa! ๐Ÿ™‡๐Ÿฝ๐Ÿ“šWasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani! ๐Ÿ‘‰๐ŸพKatika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha. ✋๐ŸพHuwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani! ๐Ÿค”Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani ๐Ÿ›ฃMtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti ๐Ÿ˜ŽUkitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze ๐Ÿ˜€๐Ÿ™๐Ÿฝ Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze ....hata mimi sijawa tajiri bado๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ‘†๐Ÿฟ Team Brayton Offical Love


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/04/mafanikio-ya-maisha-sio-elimu-tu.html

No comments:

Post a Comment