Thursday, April 23, 2020

HII INAWAHUSU WANAUME TU.

Hii inawahusu wanaume
Wanawake wengi wanalalamika kusumbuliwa na wanaume kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook.
Wanaume wengi hupenda kutongoza wanawake wa facebook iwe kwa kumaanisha au kuwatania (kujaribu kucheza na hisia). Labda niseme mwanamke akikukubalia ombi lako la urafiki haimaanishi yupo tayari kwa lolote lile utakalosema, wengine hutumia mitandao kama burudani tu sio wote hutafuta mabwana mitandaoni wengine ni wake za watu lkn still kidume unakomaa upewe namba ya simu ili iweje? Huko messenger ndio uwanja wa kuchati lkn wewe unasema hainogi kuchati huku nipe no tuchati kawaida, hivi ushajiuliza mpo wangapi huko messenger mnaodai no? atawapa wangapi hivi hiyo itakuwa ni simu au huduma kwa wateja? Mwanamke akisema hatoi no yake hebu heshimu mawazo yake lkn wengi huishia kuambulia matusi kuwa wanajiona sana.
Ndio maana wanawake ni wagumu kujibu meseji zenu sio kwamba hawapendi kuchati ila usumbufu huwa mkubwa sana, dk tatu tu za kuchati tayari unaomba no hata hamjafamiana vzr bado.
Pia namna ya kuanzisha conversation (mazungumzo) wengi hujifunga ndio maana text zinawekwa kapuni hazijibiwi. Hivi unawezaje kutxt mwanamke
"oya", "vp", "hjmb", "mzm", "hey", "nmbie"
Labda mwanamke mwizi ndio atajibu text za aina hiyo lakini kwa mwanamke anayejielewa hiyo ni dharau kubwa sana anaweza hata akakublock kabisa usimuone tena online.
So badilikeni unapomfuata mdada inbox hebu nenda kwa adabu na heshima jitambulishe kidogo, acha vimaswali vya kishamba visivyokuwa na mantiki yoyote, mfanye akuamini, mfanye akuzoee mpaka akiingia online akutafute yeye mwenyewe na asipokuona akose raha, kikubwa zaidi acha kabisa wala usijaribu kumtumia picha au video za ngono ukidhani ndio utamteka kumbe ndio unampoteza hiyo ataichukulia kama matusi na atakudharau sana. Hata ikitokea ameomba mwenyewe mwambie sina ila nitakutafutia nikutumie kama unapenda.
Kingine kitendo cha kuomba utumiwe picha wakati kwenye profile gallery yake zipo zimejaa lkn unakazania akutumie yeye hawapendagi, kuulizwa upo Whatsapp hawataki, akikutajia sehem anayoishi usitake mpaka ujue anaishi nyumba no ngap
Kama kweli kakuvutia nenda nae taratibu ukizingatia vigezo na mashart namba yake ya sm atakupa mwenyewe bila ya kuiomba


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/04/hii-inawahusu-wanaume-tu.html

No comments:

Post a Comment