WATU wengi wamekuwa wakiteseka katika uhusiano wao, wanashindwa kujua cha kufanya ili kuwa bora kwa wenzi wao.
Kila siku wanajikuta wanaingia kwenye uhusiano lakini baada ya muda mfupi unavunjika. Wapo wanaofikia hatua ya kujiapiza kwamba hawawezi kuwa kwenye uhusiano mwingine kutokana na yaliyotokea kwa wenzi waliopita – ni makosa.
Maisha hayapo hivyo, haina maana kwamba kwa sababu umeachana na fulani basi wanaume au wanawake wote watakuwa na tabia zinazofanana na aliyepita. Hayo ni mawazo mgando.
Muhimu kwako kutazama kwa kina ni pale ulipokosea. Acha kuangalia ulipoangukia, angalia ulipojikwaa. Kwanini umetengana na mwenzako? Hilo ndilo la msingi zaidi kwako.
Katika maisha huwa tunaangalia sababu za makosa, siyo makosa. Inaruhusiwa kukosea wakati wa kujifunza, lakini cha msingi zaidi ni kwa namna gani unajifunza kutokana na yaliyotokea?
Huo ndiyo msingi wa mada yetu ya leo ambayo naamini itakubadilisha kifikra.
Naamini hakuna anayependa kuachwa, lakini tukiwa tunazungumzia juu ya kuacha na kuachana ni wazi kwamba inawagusa zaidi wanawake kuliko wanaume.
Wanaume wana uwezo wa kutongoza upya na kuanzisha uhusiano mpya haraka zaidi kuliko wanawake. Hawa wamekuwa wakilia kila siku, wakati mwingine wakihisi wana mikosi au kuna mkono wa mtu.
Siyo kweli kabisa, wewe mwenyewe unaweza kuwa chanzo cha kuharibu uhusiano wako kia siku. Marafiki zangu, wanaume wanapenda kuheshimiwa, kunyenyekewa, kupendwa, kuogopwa na kupewa nafasi ya kwanza.
Hakuna mwanamume ambaye anafikiria kumuoa mwanamke mkaidi, mwanamke mkorofi, asiye na mapenzi, asiyejua thamani yake, asiyetambua nafasi yake kama mwanamke. Hakuna.
Sasa ili uweze kuwa bora zaidi katika uhusiano wako ni vyema kuwa makini sana na mambo hayo niliyoyataja hapo juu.
Ni wazi kuwa kama wewe ni kijana uliyekamilika, lengo lako hasa ni kujenga familia iliyo bora zaidi. Unatamani kupata nyumba nzuri ambayo itakuwa na furaha na siyo majonzi, kama una ndoto hizi ni vyema ukafahamu kwamba hata mwenzako (mwanamume) hatapenda kuwa na mwanamke mwenye kasoro.
Ni kweli kuwa hakuna binadamu aliyekamilika, kila mmoja ana mahali ambapo ana kasoro zake, lakini angalia sana kasoro zako zisiwe nyingi sana kiasi cha kukupotezea sifa ya kuwa mke bora.
Pengine una tatizo lakini hujui! Hebu endelea na vipengele vilivyosalia hapa chini. Je, nawe una tabia hiyo?
NI KAWAIDA KUKOSEA
Hakuna binadamu ambaye hakosei, inaelezwa kwamba, kukosea ni sehemu ya ukamilifu wa mtu. Mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema: “Ni vizuri watu wakosee ili wajifunze, huwezi kujua kitu bila kukosea, lakini unaruhusiwa kukosea mara moja tu!”
Kama ukichambua neno moja baada ya lingine ya mwanasaikolojia huyo, utaweza kuona jinsi sentesi yake fupi ilivyo na maana kubwa. Kwa manti hiyo hata kama utakosea mara mia moja, hakuna tatizo, lakini yawe makosa mapya.
Kosea kila siku, lakini kitu kipya, hii inamaanisha kwamba, kwasababu kukosea ni kujifunza, basi kama utakosea mara mia, utakuwa umejifunza pia mara mia moja. Upo hapo rafiki yangu?
Sasa wanaume wengi hawapendi wanawake ambao wanakosea na kusahau! Jenga utaratibu wa kuheshimu unachoambiwa, ukielezwa hakifai, usikaidi, huna sababu ya kuridia tena.
Kurudia kwako mara nyingi ni kuzidi kumkera mwezi wako huyo ambaye lengo lako hasa ni kuishi naye hapo baadaye. Zingatia hilo tafadhali kama kweli unahitaji kuwa na uhusiano mzuri.
MUHIMU
Kama hayo yote hapo juu yanakuhusu ni wazi kwamba unatakiwa kufanya mabadiliko ya haraka sana katika maisha yako, kama ni kweli unataka kuolewa na kudumu kwenye uhusiano wako.
Siyo rahisi mwanamume ambaye anatafuta mke akakubali kuwa katika uhusiano na mwanamke mwenye tabia zako. Tabia ni msingi bora zaidi ya uzuri wa sura na mwonekano.
Badilika. Anza taratibu, rekebisha moja baada ya lingine, halafu kuwa makini katika kila jambo, mwisho wake utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupata mwenzi wa maisha.
Usisahau kushare post hii.π Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/04/unafanyaje-unapomkosea-mpenzi-wako.html
No comments:
Post a Comment