Monday, April 27, 2020

*🍇KWENU WADADA🍇* *🍇UTUNDU NDOO HUU SIO KUJITUNDUA🍇*

TUPASHANE: Sanchi Adai Posh Queen Ni Cha Mtoto Kwake

🍇Leo nakupa utundu kidogo maana mahabba yana uhaba na uhaba usababisha ukahaba, kama ujuavyo mume ni kama sahani ya kaure inahitaji kutunzwa ili itunzike. 🍇Jitahidi ukikaribia muda wa mumeo kurudi kutoka kazini chukua maji nenda kaoge vizuri mpaka uhakikishe kijasho chote kimekatika harufu yake. 🍇Rudi chumbani kaa kitandani au kwenye dressing table uanze kujipamba, chukua poda kidogo jipake vizuri usoni kiasi uso upendeze kisha chukua wanja wako uchore kwenye nyusi na kwenye kope za juu na zachini, paka rangi midomo yako kwa ustadi wa juu, chukua manukato yako ujipake,au jifukize udi wako nzuri wenye harufu ya kuvutia,kanga nyepesi ndo vazi la kimahaba dada. 🍇Mkaribishe chakula mumeo kwa maneno ya papaso, *🎈karibu chakula mume wangu*🎈 usimuache mumeo anakula wewe ukenda jitupa chumbani au kwenye kochi la hukooo mbali naye, hasha! Huo si mwendo bibi, kaa ubavuni kwa mumeo uku anakula huku unamtupia maneno ya uchokozi,si uchokozi wa madera ulokopa laaaaa! Uchokozi wakumtoa pweza kwenye matumbawe. 🍇Jitahidi kumfanya awe mpya asahau vurugu za mchana kutwa, jifanye kama unamuhimiza kula kwa lugha ya vitendo mkatie kipande cha samaki au nyama umlishe huku wakisindikiza na maneno *🎈"kula baby mbona huli nyama"🎈* kwa sauti ya chini ya kubembeleza.mara inuka jifanye watafuta kitu mara muulize"mume wangu nikutilie juice,chungwa,ndizi,"usisubiri akujibu bibi, mume ataka kupembejewa bhana. 🍇Hakikisha akiwa anakula mshughulishe na mihuja ya kimapnzi sio unamuacha macho yapo kwenye tv anaangalia sinema zetu au tamthilia.kumbuka ndoa hujengwa sehemu mbili kubwa wakati wa kula na wakati wa kulala. 🍇Mpe maji ajisafishe mikono na umpe mumeo kitambaa ajifute akisha maliza kula, muangalie shati yake kama vishikizo bado vimefungwa, basi vifungue kwa mahaba huku unamliwaza mwambie *🎈"joto mume wangu mwili wahitaji hewa."🎈* mwache apumzike baada ya kula si kumuacha wewe utoke? Laaa! mwache kwa kumkalisha kwa mahaba


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/04/kwenu-wadada-utundu-ndoo-huu-sio.html

No comments:

Post a Comment