Wednesday, November 27, 2019

Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi Mkoani Mwanza

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza  Limefanikiwa Kuipata Silaha Moja Aina Ya Bastola Ikiwa Na Risasi Tatu  Zinatumiwa Na Wahalifu (Majambazi) Kwenye Matukio Mbalimbali Kanda Ya Ziwa  Baada Ya Watuhumiwa Wawili Wa Ujambazi Wanaume  Ambao Bado Hawajafamika Majina Wala Makazi Yao Wanaokadiriwa Kuwa Na Umri Kati Ya  Miaka 25 Hadi 30 kufariki.

Watuhumiwa Hao Walifariki Wakati Wakipelekwa Hospitali Baada Ya Majibizano Ya Kurushiana Risasi Na Askari Polisi Baada Ya Kumtishia Kumuua  Kwa Bunduki Na Baadae Kupora Pikipiki Ya ” Mwendesha Bodaboda “.

Tukio Hilo Limetokea Tarehe 26.11.2019 Majira Ya  23:40hrs Huko Maeneo Ya Sweya – Fisheries Wilayani Nyamagana, Hii Ni Baada Ya Mwendesha Pikipiki Samwel Masanja (Bodaboda)   Kuporwa Pikipiki Yake Maeneo Ya Maina Na Watu Hao  Na Baadae Wananchi Kutoa Taarifa Polisi.

Baada Ya Kupatikana Kwa Taarifa Hizo Askari  Polisi (Makachero) Walifanya Ufuatiliaji Wa Haraka Na Baadae Wakakutana Na Wahalifu  Hao Uso Kwa Uso Maeneo Ya Sweya, Walipobaini Kufuatiliwa Walianza Kuwarushia Risasi Askari  Na Askari Walijihami Na Kufanikiwa Kuwajeruhi Kwa Risasi Wahalifu Hao Ambao Baadae Walifariki Dunia  Wakati Wakipatiwa Matibabu Hospitali Ya Bugando.

Katika Eneo La Tukio Kumepatikana Bastola Moja Aina Ya Starbird Yenye Namba Za Usajili Us Patten 2563720 Pamoja Na Risasi Tatu Ndani Ya Magazine Na Pikipiki Aina Ya San Lg Nyekundu Yenye Namba Za Usajili Mc 617 Abx Ambayo Ilikua Imeporwa. Imepatikana  Miili Ya Marehemu Wote Wawili Imehifadhiwa Hospitali Ya Rufaa Ya Bugando Kusubiri Utambuzi Na Uchunguzi Wa Daktari.

Tukio La Pili.

Tarehe 26.11.2019 Majira Ya 00:05hrs Usiku Huko Maeneo Ya Kifua Wazi Barabara Kuu Ya Airport –mwanza, Kata Ya Nyamanoro, Wilaya Ya Ilemela, Jiji Na Mkoa Wa Mwanza. Abiria Mmoja Mwanamke Ambae Bado Hajafahamika Jina Wala Makazi, Anayekadiriwa Kuwa Na Umri Kati Ya Miaka 25 Hadi 30, Akiwa Amebebwa Kwenye Pikipiki Yenye Namba Za Usajili Mc 269 Bdy Aina Ya Sanya Iliyokuwa Ikiendeshwa Na Dereva Aitwaye Novart Joseph, Miaka 26, Mhaya, Mkazi Wa Jiwe Kuu – Kitangiri, Alianguka Chini Toka Kwenye Pikipiki Na Kuburuzwa Umbali Kiasi  Cha Mita 70 Baada Ya Mtandio Aliokua Amejifunga Shingoni Kuingia Na Kujisokota Kwenye Tairi (Spockert) Na Baadae Kufariki Baada Ya  Kukimbizwa Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Sekou Toure Kwa Ajili Ya Kupatiwa Matibabu. Mwili Wa Marehemu Umehifadhiwa Hospitalini Hapo Kwa Ajili Ya Utambuzi Na Uchunguzi Zaidi Wa Kitaalamu. Dereva Wa Pikipiki Anashikiliwa Kwa Mahojiano Pamoja Na Pikipiki Hiyo.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawashukuru Wananchi Kwa Kuendelea Kutoa Ushirikiano Katika Kuzuia Na Kupambana Na Uhalifu Na Wahalifu. Pia Linaendelea Kuwasihi Wananchi Wakati Wote Kuendelea Kutoa Taarifa Za Uhalifu Na Wahalifu Kwa Jeshi La Polisi Na Linawahakikishia Kushughulikia Taarifa Hizo Kwa Kuzingatia Weledi Wa Hali Ya Juu.

Aidha Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawataka Abiria Na Madereva Wa Vyombo Vya Moto Kuzingatia Sheria Za Usalama Barabarani, Hasa Waendesha Pikipiki Na Wapanda Pikipiki Wazingatie Kuvaa Kofia Ngumu Na Mavazi Ambayo Hayataleta Madhara Kwa Maisha Yao Ili Kuepusha Vifo Na Majeraha Yanayoweza Kuepukika.

Imetolewa Na

Muliro J. Muliro –ACP

Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza

27 November,2019

No comments:

Post a Comment