Wednesday, November 27, 2019

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Wakulima Kutumia Mvua Za Msimu Zilizoanza Kunyesha Na Za Vuli Kupanda Mazao Yanayokomaa Kwa Muda Mfupi.

Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb) anapenda kuwafahamisha wananchi wote hasa wakulima kutumia mvua za vuli zilizoanza kunyesha katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani na Morogoro ambayo hupata mvua mara mbili (bimodal) kwa mwaka, kupanda mazao yanayokomaa kwa muda mfupi. 
 
Wakulima wanahamasishwa kutumia vizuri mvua hizi kwa kupanda kwa wakati. Aidha, Waziri Hasunga anawaagiza Wakuu wa Wilaya kuwasimamia Maafisa Ugani Kilimo ili waweze kuwasaidia wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo kwa kupanda mbegu bora kulingana na kanda za kiekolojia na kutumia mbolea inayostahili kwenye mazingira husika.
 
Wizara ya Kilimo itaendelea kutoa ushauri wa kitaalam na maelekezo kwa wakulima na wananchi nchini kuhusu mwenendo wa mvua na hatua za kuchukua ili kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ya kutosha na hatimaye nchi kuwa na usalama wa chakula.
 
Imetolewa na:

Revocatus A. Kassimba
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Kilimo,
DODOMA.

No comments:

Post a Comment