Wednesday, November 27, 2019

Mkutano Wa 39 Wa Baraza La Mawaziri Wa EAC Kuanza Leo Jijini Arusha

Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa kwanza leo tarehe 27 Novemba 2019 jijini Arusha.

Kuanza kwa mkutano huo kunafuatia kukamilika kwa Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ulioanza tarehe 25 na kumalizika tarehe 26 Novemba 2019.

Mkutano wa Makatibu Wakuu  pamoja na mambo mengine, umejadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mapendekezo kwa mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta zinazohusiana na Jumuiya hiyo utakaoanza  tarehe 27 Novemba 2019.

Mkutano huu wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeandaliwa kwa lengo la kujadili na kukubabaliana na agenda zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Februari, 2020.

No comments:

Post a Comment