Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amempiga kijembe Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye baada ya kubwagwa kwenye Uchaguzi wa Kikanda ndani ya CHADEMA
“Nimesikia Mzee Sumaye hata Uenyekiti sijui wa “Kitongoji” wamembwaga huko Pwani, alipokuwa CCM @ccm_tanzania tulimpa kwa upendeleo Uwaziri Mkuu Miaka 10. Mzee, nadhani muda umefika huko hakuna watu, mimi na wewe tunajua imetosha. Mwenzio amepumzika na muda wa kulea wajukuu anao!” ameandika ujumbe huo katika akaunti yake ya Twitter.
Uchaguzi huo ulifanyija jana jioni Kibaha Pwani wa kumpata mwenyekiti wa Kanda ya pwani
Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Mgombea alikuwa Mzee Sumaye peke yake ndipo zikapigwa kura za ndio au hapana
Matokeo ya kura za ndio kwa Mzee Sumaye ni 28, na kura za Hapana ni 48 .Hivyo, nafasi ya Mwenyekiti bado iko wazi.
Nimesikia Mzee Sumaye hata Uenyekiti sijui wa “Kitongoji” wamembwaga huko Pwani, alipokuwa CCM @ccm_tanzania tulimpa kwa upendeleo Uwaziri Mkuu Miaka 10. Mzee, nadhani muda umefika huko hakuna watu, mimi na wewe tunajua imetosha. Mwenzio amepumzika na muda wa kulea wajukuu anao! pic.twitter.com/xfgHjI9xuf— Humphrey Polepole (@hpolepole) November 28, 2019
No comments:
Post a Comment