Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni amethibitisha amepokea barua za madiwani watano kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka ndani ya jii hilo kujiuzulu nyadhifa zao.
Mbali na barua hizo za kujiuzulu, madiwani hao pia wamemuandikia barua katibu wa CCM Wilaya ya Arusha wakiomba kujiunga na chama hicho.
Kutokana na kujiuzulu kwa madiwani hao, Jiji hilo sasa lina madiwani 28 ambapo 20 ni wa Chadema na CCM wanane.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilipata diwani mmoja lakini hivi karibuni madiwani saba wa Chadema walijiuzulu na kujiunga na chama hicho tawala.
No comments:
Post a Comment