Saturday, November 30, 2019

Mbowe Arejesha Fomu yake ya Kugombea Uenyekiti CHADEMA, Tundu Lissu Kuwa Makamu Mwenyekiti

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema atagombea Makamu Mwenyekiti wa chama hicho katika Uchaguzi unaoendelea kufanyika hivi sasa ndani ya chama hicho.
 

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe wakati akirejesha fomu yake ya kuwania Uenyekiti wa chama hicho kwa Katibu wa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini.

Mbowe amesema kuwa "Sisi viongozi tunafahamiana historia zetu na umadhubuti wetu, baada ya mashauriano tumemuelekeza Tundu Lissu ajaze fomu ya kuomba nafasi ya Makamu Mwenyekiti, na amefanya hivyo japo hatuzuii mwingine yoyote kujaza nafasi hiyo"

"Kwa sababu Prof. Abdallah Safari (Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara) anaondoka, wamejitokeza Watanzania kadhaa kujaribu kugombea nafasi hiyo, kwa kuwa tunahitaji viongozi" amesema Mbowe


Mbowe alichukuliwa fomu hiyo na wanachama waliochanga Sh1 milioni kulipia gharama na kumkabidhi. Baada ya kuipokea mbunge huyo wa Hai aliikabidhi kwa katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa.

Mara baada ya kukabidhi fomu hiyo, wanachama waliofurika katika ukumbi unakofanyika mkutano huo walishangilia

Kwa sasa chama hicho kimeingia kwenye Uchaguzi wake wa ndani ngazi ya Kikanda ambapo Desemba 18, ndiyo uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti utafanyika.

No comments:

Post a Comment