Ndiyo umeingia kwenye ndoa na mwanaume, lakini baada ya wiki mbili au mwezi unaona kashaanza kuchelewa kurudi nyumbani, unapaniki na kuanza kukagua simu yake ukidhani labda kuna sehemu anapitia, kuna mwanamke mwingine anakusaidia. Lakini ndoa yenu ni ya muda mrefu ila mlikua mnaishi mbalimbali, imetokea sasa mnaishi pamoja hata mwezi haujafika unaona kashaanza kuchelewa kurudi.
Unapaniki, unaanza kulalamika, labda kuna mwanamke ulikua unamuona naye au kuna hata meseji, kuna X wake na vitu kama hivyo, kichwani unajua kuwa alikua huko na unaanza kuona hupendwi. Inawezekana ni kweli anapitia huko, lakini nikuambie tu kuwa asilimia kubwa ya wanaume wapokua wanachelewa katika mwanzo wa ndoa zao hawaendi kwa michepuko.
Najua utashangaa lakini ndiyo ukweli, sasa unawaza kama hawaeni kwa wanawake wengine huenda wapi? Jibu ni rahisi, wanaenda kwa marafiki, wanakua na washikaji. Najua unajiuliza tena kuna nini, kwanini asikae na wewe na kufurahia wakati ndiyo kakuoa, inamaana hakupendi, inamaana hafurahii kuwa karibu na wewe? Hapana haina uhusiano na “Upendo” kuna majibu mawili katika hili.
Kwanza kabisa ni mazoea na pili ni kuboreka. Tukianza na mazoea wanaume wengi nadhani wote kabla ya kuoa walikua na tabia flani, alikua anatoka kazini kwakua nyumbani yuko peke yake basi huzunguka kwa wahsikaji, bar, nyumbani kwao au anakua kazini kufanya mambo yake. Mara nyingi hurudi nyumbani kachelewa hivyo akirudi ni kuoga na kulala.
Hata kula ilikua ni mtaani, alishakua na utaratibu huo, hivyo anapooa na kuwa kila kitu hufanyikia nyumbani basi wakati mwingine hujisahau na kuendelea kufanya mambo yaleyale kama bachela na kwakua ni mwanaume huona kama ni kawaida na anadhani kua na wewe mwanamke utaelewa. Kwakua hafanyi kitu kibaya huko anakotoka basi hajioni kama nafanya kosa, anaona si nilikua na washikaji tu, anahisi utamuelewa au hata unajua.
Katika kuboreka nikuwa alikua na mazoea hayo, sasa ameoa anarudi nyumbani anakutana na mwanamke, kila siku wanakua wanafanya kitu kilekile, anakua anaboreka, anamiss kutoka, anamiss washikaji, anamiss kila kitu hivyo anataka kupumua. Akiwa hajui kuwa hata mkewe naye anamiss hivyo vitu anaamua kutoka, kwenda kupumua anakuacha mwanamke wewe unawaza kwanini hataki kuwa karibu na mimi?
Hapo yeye haoni kama anafanya kosa, lakini anashangaa ghafla mwanamke unaanza kulalamika, unaanza kuongea, kwakua yeye hajioni kama anafanya kosa basi hukuona wewe kama una kisirani, unataka kumpangia maisha, unataka kumtawala. Unapomuambia hutaki awe na marafiki flani kwakua hawajaoa na wanamharibu anakushangaa kwani alikua nao hata kabla ya kukutana na wewe lakini akaamua kukuoa.
Sasa swali linakuja, je ni wakati gani ambapo mwanaume huanza kuechelewa kwaajili ya kuchepuka? Hapa nataka muwe makini, sisemi mume wako hachepuki kwakua inawezekana umefumania meseji, lakini mara nyingi mwanzo wa ndoa kuchepuka sio kunakomfanya achelewe kurudi, sababu nishazitaja hapo. Anaanza kuchelewa kwa kuchepuka pale ambapo nyumba inazidi kuwa na kelele.
Kwamba yuko mtaani amepiga stori na washikaji anataka kurudi nyumbani, lakini anakumbuka kuwa mkewe ni kichomi, kwamba akifika atasomea risala ya makosa ya tangu wanakutana na hata ya ma X wake. Lakini kule mtaani nako washikaji washaondoka amebaki mwenywe, akili zake fupi zinamuambia ni heri akatafute faraja, labda kwa X wake, kamchepuko kake kazamani au mtu mpya.
Hii ni kwasababu mwisho wa siku atahitaji mwanamke, mwanamke ambaye wanaweza kuongea naye, kucheka naye bila malalamiko, bila kununa, anaona anapata faraja kumbe anaharibu ndoa yake na kuzidi kumfanya mkewe kuwa na kisirani. Hapo ndiyo huanza kuchepuka na huona kama kuchepuka ndiyo kitu cha kawaida, anaona kama mkewe hawezi kumpa furaha ambayo anapewa na mchepuko kumbe hajaamua kuitengeneza tu.
Hajui kama angewahi tu huyo mkewe aisingekua na hicho kisirani na wangekua na amani. Sasa dada zangu kama uko katika hali hii, mume ndiyo mpya au ndiyo mmeanza kuishi pamoja, hembu ondoa akili zako katika kuchepuka. Hachelewi kwakua anachepuka. Hata kama ana mchepuko lakini mara nyingi hukutana nao mchana au hata huwahi kuondoka hivyo hicho unachokilalamikia kila mara ndiyo kitamfanya kuhamia kwa huo mchepuko ili kupunguza stress unazompa.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/04/mjue-mume-wako-mara-nyingi-kuchelewa.html
No comments:
Post a Comment