Tuesday, April 7, 2020

KWENYE MAHUSIANO LAZIMA UYAFAHAMU HAYA!

πŸ“‚Kwenye mahusiano, Ukitambua kuwa kuna kukosea na kukoseana. Basi neno msamaha na samahani lazima liwe silaha ya upendo wenu.
πŸ“‚Kwenye mahusiano ukitambua hakuna mkamilifu kati yenu basi Huruma na Kuhurumiana iwe nguzo ya upendo wenu.
πŸ“‚Kwenye mahusiano ukitambua kuna kupewa na kupeana basi neno Asante liwe shina la upendo wenu.
πŸ“‚Kwenye mahusiano ukitambua kwamba kuna kupata na kukosa basi subira itumike kulinda upendo wenu.
πŸ“‚Kwenye mahusiano ukitambua kuna kuanguka na kusimama basi busara iwe mhimili wa upendo wenu

Image may contain: one or more people and wedding


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/04/kwenye-mahusiano-lazima-uyafahamu-haya.html

No comments:

Post a Comment