Tuesday, April 21, 2020

HILI NDILO JAMBO WANAUME WENGI HAWALIFAHAMU KUHUSU WANAWAKE

MWANAMKE na mwanamume kila mmoja ana udhaifu wake. Katika suala la mahusiano, kati ya madhaifu ya wanaume ambayo wanawake wengi wanaonekana kukubaliana nayo ni pamoja na kunyenyekewa, kusikilizwa na tamaa ya tendo la ndoa.
Japo tendo la ndoa ni mada pana sana ila kwa mwanamume hili suala ni la kipaumbele sana. Mwanamke ana uwezo wa kukaa muda mrefu bila ngono.
Ila si kwa mwanamume. Mwanamume kutokana na uasili wake, anapenda sana ngono na kwake ngono si suala linalotafsiri upendo muda wote.
Anaweza kufanya ngono na watu kadhaa na bado akawa na hisia za upendo juu ya mtu mwingine. Kwa mwanamke kuna utofauti kidogo.
Kwa mujibu wa tafiti kadhaa, japo mwanamke naye anaweza kufanya ngono na mwanamume mwingine kwa sababu kadhaa na asiwe na hisia nao ila wanawake wengi hufanya ngono na watu wenye hisia nao za kimapenzi.
Wanawake wengi huwa hawaridhiki wala kujihisi fahari kufanya ngono na mwanamume asiye na hisia naye. Miongoni mwa madhaifu ya wanawake katika mapenzi na huu ni udhaifu wa asili ni kubembelezwa, kujaliwa na kupatiwa iwe zaidi, sifa ama matumizi.
Huu ni miongoni mwa dhaifu kubwa za wanawake. Dhaifu hizi si kitu cha kujitakia, ni suala la asili. Kama ambavyo wanaume kupenda ngono ni suala lao la kiasili pia wanawake kupenda kuhudumiwa na kupewa ni suala lao la kiasili.
Ila hapa kuna tatizo. Wakati wanawake wamekubaliana na ukweli kwamba ngono ni udhaifu wa wanaume ila wanaume wengi bado hawajakubaliana kwamba kupewa ni udhaifu wa wanawake.
Mwanamke kumpenda mwanamume maana yake si kuwa hatahitaji kupewa ama kuletewa zawadi, hapana. Upendo wa mwanamke kwa mwanamume utamfanya amnyenyekee, amheshimu, kujitoa kwake na kuwa mvumilivu.
Mwanamke kupewa kitu ama vitu na mwanamume kwake ni ishara ya kuthaminiwa, kukumbukwa na kujaliwa. Na zawadi kwa mwanamke si lazima kiwe kitu kikubwa sana. Hapana. Zawadi ni kitu chochote chenye maana.
Wanaume wanatakiwa kufahamu kuwa mwanamke anapotaka kitu si kwamba ‘anawachuna’, hapana. Huo ni udhaifu wake.
Kitu ambacho wanaume wanatakiwa kufanya si kulalamika ama kudhani wanaonewa. Wanatakiwa kuwa wabunifu zaidi katika mahusiano yao pamoja na kuwa tayari kutoa zawadi kwa wapenzi wao.
Unapokuwa mbunifu hata kumfanyia mambo mengine mazuri na ya kumfurahisha, si tu atakuwa na amani na wewe ila pia atakuwa na wigo mpana wa kukufikiria.
Mwanamume inabidi aelewe kama ilivyo yeye, mwanamke pia ana udhaifu wake. Na njia nzuri ya kuishi naye juu ya madhaifu yake haya si kulalamika ila ni kumfanyia vingi vya kumfanya asifikie tu upande mmoja wa udhaifu wake.
Ikumbukwe tu ikiwa mtu katika uhusiano hakutani na vitu vingi vipya vya kumfurahisha na kumpa raha, ni lazima tu fikra na akili yake yote iegame kuwaza udhaifu wake.
Mwanamke anaweza kutosukumwa sana na udhaifu wake wa kuwaza kuhudumiwa na kupewa ikiwa mwanamume aliye naye atakuwa mbunifu na kumpa vitu vingi vya thamani na maana katika maisha yake.
Ifahamike kadiri unavyoshindwa kuwa mbunifu, ndivyo unavyozidi kumfanya mpenzi wako awe na fikra juu ya udhaifu wake.
Wakati mwingine mwanamke wako anaweza anataka tu kupewa zawadi na fedha kwa sababu toka awe na wewe hakuna kitu kingine cha maana unachompa zaidi ya zawadi na fedha.
Mwenzako ili aweze kuwa vile unavyotaka na kupunguza nguvu ya udhaifu wake inabidi umwoneshe mambo mengine ya kufurahi na kumpa raha.
Ukishindwa kufanya hivyo basi atasukumwa na vile vitu ambavyo kiasili ndio udhaifu wake. Wanaume wanatakiwa kutambua kwamba wanaweza kupunguza ukubwa wa kuombwa fedha na vitu vingine ikiwa watakuwa na vitu vingine vizuri vya kuwapa wanawake zao.
Kama tulivyoona kiasili mwanamke ni kiumbe mwenye kuhitaji kupewa na kuhudumiwa ila pia ni ukweli kwamba wapo wengine katika uhusiano wanaomba zaidi fedha na zawadi kuliko wengine. Unajua sababu ni nini?
Sababu kubwa ni mazingira na namna wanavyotendewa na wenzao. Mwenzako unamtendea nini? Kama huna kipya, humfurahishi, kwanini asiwaze zawadi na fedha tu ambacho ndiyo kitu kiasili kimfurahishacho kwa urahisi?
Maisha ya kimahusiano ni hesabu ya kuishi na mwenzako. Kama hujui hesabu nzuri ya namna na hakucheza na fikra na hali ya matendo ya mwenzako jua umepotea.
Mwanamke ana haki ya kuomba kwa sababu hilo ni suala la kiasili kwake. Kama wewe hutaki kuombwa mara kwa mara inabidi umpe mwenzako sababu ya kutofanya hivyo kwa kumpa mbadala wa mambo hayo yatakayompa amani, raha na uchangamfu.
Usimwite mwanamke kuwa ana tamaa akiomba kitu. Jiulize sababu ya yeye kuomba na jukumu lako kwake. Ingawa pia ni kweli wapo waombaji ombaji ovyo ila pia wapo wengi wanaomba kwa sababu kuu mbili.
Kwanza, sababu ya shida na kwa kuwa anakuamini haoni aibu kukuomba msaada. Pili, ni kwa sababu za kiasili. Mwanamke hupenda kupewa. Kwake kupewa ni alama ya kujaliwa, kuthaminiwa na kufikiriwa zaidi.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/04/hili-ndilo-jambo-wanaume-wengi.html

No comments:

Post a Comment