Monday, July 13, 2020

Ujumbe wa Mourinho kwa Arteta Baada Kulazwa na Tottenhum


Jose Mourinho lands new job - AS.com

Mikel Arteta alichukua uongozi wa Arsenal Disemba 2019 akimridhi Unai Emery baada ya kuachiliwa kazi

Arsenal inashikilia nafasi ya 10 katika ligi huku matokea yake ikizidi kusambaratika

Jose Mourinho amemnyeshea sifa Mikel Arteta hata baada ya kuonyeshwa adabu ya mabao 2-1 na klabu ya Tottenham Jumapili, Julai 12.

Licha ya Arsenal kutamba katika mechi hiyo kwa dakika 90, Spurs bado ilipata tabasamu kwa kuokota pointi zote tatu.

Arsenal ilijipa bao la kwaza kunako dakika ya 16 kupitia kwa Alexander Lacazette, bao ambalo lilisawasishwa muda mfupi baadaye na Son Heung-Min.

Toby Alderweireld aliipa Tottenham bao la ushindi baada ya kuandaliwa pasi safi ya kona na Heung-Min.

Matokeo ya mechi hiyo iliipigisha hatua Tottenhum hadi nafasi ya tisa kwenye ligi huku Arsenal ikisalia kwa pigo.

‘’Nadhani mechi hiyo ilikuwa ya akili sana,  naamini Mikel alipata njia ya kuwawezesha kucheza na kujiimarisha. Wanaimarika,’’ Jose aliandika.

Ni wazi kuwa Arteta angali ana kibarua kigumu katika kuirudisha klabu ya Arsenal alikoiacha Jose baada ya kuiridhi kwa Umai Emery.

Mikel Arteta alichukua uongozi wa klabu ya Arsenal 2019 akimridhi  Unai Emery.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/13/ujumbe-wa-mourinho-kwa-arteta-baada-kulazwa-na-tottenhum/

No comments:

Post a Comment