Sunday, July 12, 2020

Dondoo za leo: Membe kuelekea ACT Wazalendo, Upinzani wataka rais ajiuzulu, Cheyo aomba kongamano kwa JPM

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Mmebe kutimkia ACT Wazalendo, Upinzani wataka rais ajiuzulu na mwisho ni juu ya Cheyo kutaka kongamano la vyama vya siasa.

MEMBE KUELEKEA ACT WAZALENDO

SASA ni dhahiri kuwa Bernard Kamilius Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa nchini Tanzania, yuko mbioni kujiunga na ACT – Wazalendo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wandamizi wa ACT- Wazalendo zinasema, majadiliano kati ya mwanasiasa huyo na viongozi hao juu ya kujiunga kwake na chama hicho, tayari yamekamilika.

Soma zaidi>>>

UPINZANI WATAKA RAIS AJIUZULU

Viongozi wa upinzani nchini Mali wamemtaka rais Ibrahim Boubacar Keita kujiuzulu , baada ya kukataa makubaliano yaliolenga kuzuia machafuko yanayoendelea nchini humo.

Takriban watu wanne waliuawa wakati wa maandamano siku ya Ijumaa , na kulikuwa na makabiliano zaidi siku ya Jumamosi.

Maandamano hayo yalimlazimu rais kufutilia mbali mahakama kuu ambayo imekuwa katikati ya mgogoro huo baada ya kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi mwezi Machi.

Soma zaidi>>>

CHEYO AOMBA KONGAMANO LA VYAMA VYA SIASA

MWENYEKITI wa Chama cha UDP, John Cheyo, amemshauri Rais Magufuli, kufikiria uwepo wa kongamano la vyama vya siasa nchini ambalo litajumuisha vyama vyote vya upinzani kwa lengo la kujadili masuala muhimu ya Kitaifa.

Mbali na hilo, pia mwenyekiti huyo amemuomba Rais Magufuli kuwezesha kuwepo kwa uwakilishi wa wabunge wakulima watakaopaza sauti kwa ajili ya wakulima wa mazao mbalimbali yanayoulimwa nchini ili yaweze kuuzwa kwa bei nzuri na mkulima afaidike.

Soma zaidi

Tukimalizia dondoo hebu tuangalie japo kwa ufupi dhana hii iliyojengeka kuwa ili uwe tajiri lazima ujitenge na matendo ya huruma na uwe katili licha ya kuwepo kwa dhana nyingine inayokindhana na hii.

Hebu tuangalie hapa hoja za mdau;

Mdau kutoka mtandaoni anadai ili uweze kuwa tajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya huruma, utu, wema na ushikamane na Ulimwengu wa giza, dhuluma na uwe katili japo kwa kificho, Lakini kuna wengine wamejichumia mali kwa kufuata njia zinazokubalika kisheria na kidini pia.

Anadai, itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi, uuze kwa faida kubwa. Uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako

Lakini pia mdau anaeleza kuwa itabidi ununue hata kuuza mali za wizi au magendo ili usitetereke kiuchumi. Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi. Ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri

Aidha, Mdau anadai ukiwa tajiri, kwa kiunafiki na kuficha makucha yako utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii

Je, una maoni gani kwenye hoja hii ya mdau?



source http://www.bongoleo.com/2020/07/13/dondoo-za-leo-membe-kuelekea-act-wazalendo-upinzani-wataka-rais-ajiuzulu-cheyo-aomba-kongamano-kwa-jpm/

No comments:

Post a Comment