
Kampuni moja la India, India Biocon Ltd imepata ruksa ya kutumia dawa zake katika kutibu wagonjwa. Picha:Hisani.
Janga la virusi vya corona si neno geni tena, limeteketeza mataifa, si uchumi, si miundo msingi, kila sekta na kila nchi inalia kufuatia kulipuka kwa virusi hivyo.
Wanayansi wamekesha usiku kucha na mchana kutwa mahabarani katika juhudi za kutafuta suluhu la kudumu kwa janga hili, mwanga sasa ukionekana kutokea.
Kampuni moja la India, India Biocon Ltd imepata ruksa ya kutumia dawa zake katika kutibu wagonjwa waliombukizwa virusi vya corona.
Kwa mujibu wa jarida la Reuters, kampuni hiyo ilieleza kupitia kwa taarifa Jumamosi, Julai 11 kuwa wamepewa idhini ya kutumia dawa zao aina ya Itolizumab kuwatibu wagonjwa wa covid19.

Kulingana na afisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo, dawa hiyo ilithibitishwa na bodi ya kudhibiti madawa DCGI baada ya kujaribiwa na kuonyesha uwezo wa kutibu virusi hivyo vya corona.
Majaribio hayo yalionyesha asilimia kubwa ya wagonjwa wa corona waliotumia dawa hiyo wakipona.
“The randomised control trial indicated that all the patients treated with Itolizumab responded positively and recovered,” Kiran Mazumdar-Shaw.
‘’ Randison control trial ilionyesha kuwa wagonjwa wote waliotibiwa kwa Itolizumab walipona,’’ Kiran Mazumdar-Shaw, afisa mkuu wa India Biocon Ltd mtendaji alisema.
Kando na virusi vya corona, imebaini kuwa dawa hiyo pia hutibu magonjwa ya ngozi.
Hatua hii inajiri siku chache tu baada ya bilionea Bill Gates kudai kuwa mipango ya kumaliza kabisa janga la corona ipo njiani..
source http://www.bongoleo.com/2020/07/13/habari-njema-kwa-dunia-suluhu-la-covid19-latangazwa/
No comments:
Post a Comment