Monday, July 13, 2020

Mkurugenzi NEC Awajibu Wanaodai Tume Huru


Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi nchini (NEC) Dr Wilson Mahera amesema baadhi ya vyama vya upinzani ambavyo vinalalamika juu ya tume huru ya uchaguzi havina ajenda ndo maan wanalalamika.

Akizungumza Kwenye mahojiano na kituo cha Clouds Fm Dr Mahera amesema tume huyo haijalalamikiwa kwanzia ilipoundwa mwaka 1963 imesimamia chaguzi zote bila kulalamikiwa.

“Tume iko huru na imeazishwa mwaka mwaka 1993 na wakati huo wote imekuwa ikisimamia uchaguzi na hakukuwa na malalamiko lakini sasa hivi ndio unasikia malalamiko nadhani hao wanaolalamika wamekosa ajenda” amesema

Ikumbukwe mapema Julai 7, 2020 vaadhi ya wanarakati kwenye mitandao ya kijamii walianzisha harakati ya kudai tume huru ya uchaguzi walioiita jina la 77nyeupe.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/13/mkurugenzi-nec-awajibu-wanaodai-tume-huru/

No comments:

Post a Comment