
Klabu ya Manchester City inatarajia kuendelea kushiriki michuano ya UEFA msimu ujao baada ya kufanikiwa kushinda rufaa dhidi ya Shirikisho la soka barani ulaya.
Man City ilihukumiwa mapema mwaka 2019 kutoshiriki michezo ya UEFA kwa misimu miwili kutokana na kuvunja kipengele cha matumizi mabaya ya pesa.
Baada ya kuhumiwa man city ilikata rufaa juu ya hukumu hiyo kwenye mahakama ya rufaa ya maswala ya michezo (CAS) na leo Julai 13,2020 kufanikiwa kushinda rufaa hiyo.
Man city ambayo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu England imejihakikishia kucheza michuano hiyo msimu ujao kutokana kujikusanyia pointi nyingi nyuma ya vinara Liverpool.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/13/man-city-washinda-rufaa-kukipiga-uefa-mwakani/
No comments:
Post a Comment