Monday, July 13, 2020

Chelsea Yataja Mchezaji Wanaotarajia Kumuuza Ili kumsaini Nyota wa Ujerumani

N'golo Kante: Chelsea to sell Frenchman to Real Madrid and raise funds for Havertz deal

Chelsea inatazamia kuchanga hela kumsaini Kai Havert. Picha;Hisani

Ng’olo Kante huenda akaigura Chelsea hivi karibuni na kujiunga na Real Madrid

Kante alihamia Stamford Bridge 2016 baada ya kuisadia Leicester kujinyakulia ushindi wa ligi ya premia kwa mara ya kwanza kabisa

Mkuu wa klabu ya Chelsea Frank Lampard hadi sasa ni wazi kuwa amemaliza mipango ya kumruhusu N’golo Kante kujiunga na klabu ya Real Madrid  kama njia ya kuchanga hela tayari kumsaini  Kai Havetz.

Klabu hiyo tayari imekamilisha dili ya kumsaini Hakim Ziyech wa Ajax pamoja na  Timo Werner wa RB Leipzig shughuli iliyogharimu £85.

View this post on Instagram

An excinting end of season @chelseafc 🔵🔵

A post shared by N'Golo Kanté (@nglkante) on

Kando na hivyo, iwapo Chelsea itahitaji kuwasaini wachezaji zaidi, italazimika kuwauza wachezaji wengine kufunga dili.

Kwa mujibu wa jarida la SunSport, nyota wa Bayer Leverkusen yuko tayari  kuihama klabu yake, Stamford Bridge ikiwa mbioni kumnyakua.

Chelsea italazimika kufikia gharama ya £90 milioni kabla ya klabu yake kumruhusu kuondoka.

Nyota huyo wa Ufaransa ni mmoja wa wachezaji ambao wameweza kushinda ligi ya premia akichezea klabu mbili tofauti mtawalia na hata kuibuka mchezaji bora wa msimu.

Kante ameonyesha ugwiji si kwa kuchezea kiungo cha ulinzi tu bali pia kati.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/13/chelsea-yataja-mchezaji-wanaotarajia-kumuuza-ili-kumsaini-nyota-wa-ujerumani/

No comments:

Post a Comment